BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKELEWA NA WAZEE WAKATI AKIHAMIA RASMI MKOANI DODOMA


Kikundi cha ngoma cha JKT kikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amehamia rasmi Dodoma leo Ijumaa Septemba 30, 2016.

Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehamia rasmi mkoani Dodoma Ijumaa Septemba 2016.

Majaliwa ametua katika uwanja wa ndege wa Dodoma saa 10.07 jioni akiwa ameongozana na mkewe na kupokewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Walemavu, Jenester Mhagama.

Baada ya kuwasili alikwenda moja kwa moja kwenye makazi yake mpya yalioko Mlimwa ambako alipokewa na wazee wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wa dini. 


Katika Barabara inayoelekea kwenye makazi yake, wakazi wa Dodoma wamesimama kandokando wakimshangilia wakimpungia majani ya miti kama ishara ya amani huku katika lango la kuingilia nyumbani kwake, kukiwa kumejaa Bajaji na pikipiki.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: