TETEMEKO LA ARDHI LAWASOMBA MKURUGENZI, KATIBU TAWALA NA MHASIBU MANISPAA YA BUKOBA
Viongozi wa juu watatu wa mkoa wa Kagera wanaotuhumiwa kufungua akaunti feki yenye jina la ‘Kamati ya Maafa kagera’ kwa ajili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mahakama ya Hakimu Mkazi, mjini Bukoba leo.
Viongozi hao ambao wanatuhumiwa ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba,Steven Makonda na Mhasibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Simbaufoo Swai.
Mashtaka yanayowakabiri ni kudaiwa kula njama pamoja na kufungua akaunti feki na kutumia vibaya madaraka vyao.
Viongozi hao walisimamishwa kazi juzi kwa kosa la kufungua akaunti feki yenye jina kama linalotumiwa na akaunti ya serikali kwa ajili ya kupokea misaada ya waathirika wa maafa ya Kagera ‘Kamati ya Maafa Kagera’ yaliyotokea hivi karibuni mkoani humu.
Hatua imekuja baada ya kufungua akaunti kwa ajili ya kukusanya michango ya fedha ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililohusisha vifo cha watu 17 kupoteza maisha na kujeruhi zaidi 250 nyumba, ofisi za serikali na taasisi kuharibiwa pamoja na miundombinu ya barabara.
0 comments:
Post a Comment