BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AMIRI JESHI MKUU RAIS MAGUFULI ALIPOFUNGA MAFUNZO YA MEDANI YA KIJESHI MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ BAGAMOYO.


Kiongozi wa ndege vita akitoa saluti maalumu kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais DKT John Magufuli wakati wa
kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange alipowasili kushuhudia kufungwa kwa mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Robert Mboma.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa (kushoto). Sehemu ya ndege vita.
Vifaru vinavyotembea majini na ardhini vikikaribia ngome ya adui.
Vifaru vinatoka majini na kuendelea na mashambulizi nchi kavu.

Hali tete ngome ya adui.

Makamanda wakiwasiliana na walio uwanja wa vita.  Amiri Jeshi mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea jambo na Mkuu wa Majeshi Jemerali Davies Mwamunyange.
Meza kuu ikibadilishana haya na yale.
Hatimaye zoezi la kumtoa adui limekamilika kwa mafanikio na wapiganaji wanaelekea uwanja wa sherehe.
Wapiganaji wanarudi kishujaa.
Furaha ya ushindi baada ya mapambano ya anga, majini na ardhini. Bendi ya muziki ya JWTZ Mwenge Jazz Band “Wana Paselepa” ikitumbuiza wimbo wa mashujaa
Amiri Jeshi Mkuu anajiunga kunogesha burudani wakati Bendi ya muziki ya JWTZ Mwenge Jazz Band “Wana Paselepa” wakati ikitumbuiza wimbo wa mashujaa  Amiri Jeshi Mkuu akiongea na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
Ndege vita zikipita kwa mara ya mwisho
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akikabidhi bendera kwa mpiganaji kuirudisha makao makuu kuashiria hitimisho la zoezi hilo.
Mkuu wa majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akisoma risala yake.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Husssein Mwinyi akisoma hotuba yake na kumkaribisha viongozi wakuu kuongea na wapiganaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea na wapiganaji.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wapiganaji. Vifijo kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo katika hotuba yake.
Amiri Jeshi Mkuu akiagana na wapiganaji. Safi sana….
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiondoka eneo la tukio kwa ukakamavu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: