MKUU WA WILAYA AMSWEKA NDANI YA MAHABUSU AFISA MIFUGO WA KATA SENGEREMA
Buchosa. Mkuu wa Wilaya Sengerema, Emmanuel Kipole ametoa agizo la kuwekwa ndani kwa Ofisa Mifugo Kata ya Bukokwa wilayani hapa, Rajabu Sangwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kutoa vibali vya kusafirisha mifugo kwa wafanyabiashara kinyume na utaratibu.
Akitoa agizo la kukamatwa ofisa huyo, Kipole alisema watumishi wanaotumia madaraka yao vibaya hawataonewa huruma bali watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kujibu tuhuma.
Kipole alitoa wito kwa kwa watumishi wa Serikali kutimiza wajibu wao kuwasaidia wananchi.
Mkazi wa Kata ya Bukokwa, Juma Samsoni alisema doria iliyofanywa na mkuu wa wilaya imebaini mambo mengi ikiwamo kukamata watu wanaojihusuisha na uvuvi haramu, magari yanayosafirisha mazao ya misitu usiku kinyume na utaratibu.
0 comments:
Post a Comment