AFUNGWA MIAKA 30 JELA KIUZEMBE
Dar es Salaam. Hatua ya kujitoa akili kwa Nicolaus Edward na kuamua kumbaka mtoto wa miaka sita, kumesababisha Mahakama ya Wilaya ya Ilala kumzawadia kifungo cha miaka 30 jela.
Pia, imemuamuru Edward ambaye alikuwa mkazi wa eneo la Nyuki lililopo Majohe, kumlipa mtoto huyo fidia ya Sh5 milioni atakapomaliza kutumikia kifungo chake.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Maua Hamduni alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na vielelezo vilivyowasilishwa.
“Nimeridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na vielelezo viwili vilivyotolewa na daktari, hivyo mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa wanaume wengine, pia anatakiwa kumlipa fidia ya Sh5 milioni mlalamikaji atakapomaliza kutumikia kifungo chake,” alisema Hakimu Maua.
0 comments:
Post a Comment