BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU MIL 8 WAJIUNGA NA HUDUMA ZA KIBENKI KUTUMIA SIMU ZA MKONONI TANZANIA


Idadi ya watumiaji wa huduma za fedha kwa kutumia simu za mkononi nchini imepaa kwa asilimia 4.6 baada ya watu zaidi ya 800,000 kujiunga na huduma hizo katika robo ya pili ya mwaka huu licha idadi ya watumiaji huduma za simu kuporomoka.

Takwimu zilizotolewa leo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwa hadi Juni mwaka huu kulikuwa na watumiaji wa huduma za fedha kupitia simu za mkononi milioni 17.33 ikilinganishwa na watu milioni 16.53 waliorekodiwa Machi.



Ongezeko hilo linaonyesha mwamko mkubwa katika upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia mfumo wa dijitali unaokua kwa kasi ulimwenguni.

Takwimu hizo zilizowekwa katika tuvuti ya TCRA, zinaeleza kuwa hadi kufikia Machi kulikuwa na watumiaji wa huduma za simu milioni 39.57 lakini idadi hiyo ilianza kushuka taratibu hadi kufikia milioni 38.6

Katika kipindi hicho kulikuwa na kampuni nne za simu zilizokuwa zikitoa huduma za kifedha ambazo ni Vodacom (Mpesa), Tigo (Tigo Pesa), Zantel (Ezy Pesa) na Airtel ambayo hutoa huduma hizo kwa jina la Airtel Money. 


Hata hivyo, katika kipindi hicho cha Aprili hadi Juni mwaka huu, idadi ya watumiaji wa huduma za simu hususan sauti, ilionekana kushuka kwa wastani wa laini 300,000 hata kabla ya siku ya mwisho ya uzimaji simu bandia kufikia Juni 17.

miezi miwili baadaye.
Tofauti na ambavyo wengi wangetarajia kuwa uzimaji wa simu bandia uliofanyika Juni ungepunguza watumiaji, hali ilianza kuimarika baada ya idadi hiyo kuanza kupaa kufikia watumiaji milioni 39.2 mwezi huo, kiwango ambacho bado kilikuwa chini ya kilichorekodiwa Machi.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: