BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALIMU WALIOMTANDIKA MAKOFI MWANAFUNZI SEKONDARI MBEYA DAY WALIKUWA KATIKA MAFUNZO KWA VITENDO

Tokeo la picha la photos of viboko mwalimuMwalimu akitoa adhabu ya kiboko kwa mwananfunzi.

Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya walimu wa shule ya Mbeya Day wanaodaiwa kumshushia kipigo mwanafunzi, MKuu wa Shule na baadhi ya walimu wamechukuliwa na polisi kwa mahojiano asubuhi leo.

Hatua hiyo imekuja baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu, Sebastian Chinguka akipigwa kikatili na walimu. 


Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 28 baada ya mwanafunzi huyo kutofanya zoezi la somo la Kiingereza. Zinaeleza kuwa walimu waliofanya kitendo hicho walikuwa kwenye mafunzo kwa vitendo.

Taarifa ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla imeelezea namna tukio lilivyoanza.

Taarifa ya awali ya tukio la kupigwa mwanafunzi wa Mbeya Day ndugu, Sebastian Chingulu.

Tukio lilianza tarehe 26/9/2016 mwalimu Frank Msigwa mwanafunzi kwa vitendo toka chuo kikuu cha Dar Es salaam kutoa assignment ya soma la kingereza kwa wanafunzi wa kidate cha Tatu.


Baada ya kusahihisha aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya na tarehe 28/9/2016 alikwenda darasani na kutoa adhabu na alianza kwa kuwapa adhabu ya push up, kupiga magoti na baadae viboko viwili katika utekelezaji huo mwanafunzi Sebastian Chingulu alikataa kufanya kutokana na kuumwa na goti.


Kufuatia kukataa adhabu mwalimu, Frank Msigwa na wenzake wawili, John Deo na Sanke Gwamaka walimpeleka ofisini na kuanza kumshambulia kwa kipigo na baada ya tukio hilo walitoeka na wakati wanamshambulia mwalimu mwingine aliwasihi wasimpige na alirekodi tukio hilo.


Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu na mwalimu mkuu kwa mahojiano, kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu na mwanafunzi aliyepigwa.


Nawahakikishia serikali itawasaka popote walipo walimu hawa waliofanya tukio hili na kufikishwa katika vyombo vya dola na sheria.


Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa na matibatbu
hii ni taarifa ya awali nitaendelea kutoa taarifa kwa kila hatua
Amos G Makalla
Rc Mbeya
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: