BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA POLISI WA USALAMA KUFYATUA RISASI NA MABOMU YA MOSHI


Ripoti kutoka eneo la kati la Ethiopia, zinasema kuwa kumetokea ghasia nyengine baina ya askari wa usalama na waandamanaji wanaopinga serikali, na watu kadha wamekufa katika mkanyagano.

Shirika la habari la Reuters, limewanukuu walioshuhudia tukio hilo, wakisema kuwa polisi walifyatua risasi na moshi wa kutoa machozi, wakati wa sherehe katika mji wa Bishoftu, jimbo la Oromiya.

Haijulikani kama kuna maafa yoyote yaliyotokea.

Eneo hilo pamoja na jimbo jirani la Amhara, yamekuwa na mapambano kwa miezi kadhaa na mamia ya watu wameuwawa huku watu wa huko wanazidi kuandamana kupinga kile wanachosema, ukandamizaji unaozidi kufanywa na serikali.

Wakuu wanasema maandamano hayo yanachochewa kutoka nchi za nje.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: