BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DONALD TRUMP AMALIZA KESI KWA KULIPA DOLA 25 MIL

Wakili wa rais mteule wa Marekani Donald Trump ametatua kesi ya mamilioni ya madola iliyokuwa inamkabili mteja wake ili apate nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya na kuangazia changamoto zinazoikabili Marekani.
Wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezajiWanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji 

Trump alikuwa ameshtakiwa na wanafunzi wa zamani kwa ubadhirifu wa pesa katika chuo kikuu cha Trump, ambapo wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji

Rais huyo mteule amekuwa akikanusha madai hayo lakini hatimaye ameamua kulipa dola milioni ishirini na tano ili kumaliza kesi hiyo. Mpango huo hata hivyo haumuhitaji kukiri kwamba alifanya makosa.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment