BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIZUKA YAIZUIA GAIRO DC LIGI DARAJA LA TATU 2016/2017 HATUA YA SITA BORA MOROGORO


Juma Mtanda, Morogoro.
Ndoto za timu ya Gairo DC FC kuwania ubingwa wa ligi daraja la tatu 2016/2017 zilitumbukia nyongo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 mbele ya Kizuka FC katika michezo ya hatua ya sita bora ya ligi hiyo inayoendelea kufanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Kizuka FC inayomilikiwa na kikosi cha urushaji wa ndege cha JWTZ ilizima furaha ya Gairo DC FC dakika ya 88 kufuatia mshambuliaji, Ibrahim Shabaan kuisawazishia timu yake bao kufuatia kufungwa bao la mapema dakika ya sita na wapinzani wao.

Mshambuliaji huyo alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira wa juu uliopigwa na, Lucas Nivako na kumzidi maarifa kipa wa Gairo DC na kupiga mpira kwa kichwa na kujaza mpira wavuni na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya bao 1-1.

Bao la Gairo DC FC lilifungwa na mshambuliaji, Emmanuel Tuji kufuatia safu ya ulinzi wa Kizuka FC kuzembea kuondoa mpira uliokuwa eneo la hatari uliopigwa na Mamboleo Dongo na kujikuta ikiaga kuwania ligi hiyo.

Gairo DC FC iliyotumia muda mwingi kujilinda zaidi baada ya kupata bao la kuongozi, washambuliaji wa Kizuka FC, Kenedy Bago, Mohamed Nampoka na Mushika Juma walipoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga mabao lakini mipira hiyo iliishia mikononi mwa kipa wa Gairo DC FC.

Leo jioni timu ya Black Viba FC na Mzinga FC zitachuana kufa na kupona kuhakikisha moja wapo inapata matokeo ili kuungana na timu ya Shupavu FC iliyotangulia hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo miwili katika kundi A.

Baada ya Kizuka FC kupata sare hiyo dhidi ya Gairo DC FC tayari imeingia hatua ya nusu fainali huku ikiwa imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Moro Kids FC yenye pointi tatu katika kundi B.


Michezo ya hatua ya sita bora inatarajia kufika tamati kesho Novemba 14 mwaka huu kati ya Kizuka na Moro Kids.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: