Mshambuliaji wa timu ya soka ya Kupamba na Ujambazi FC, Fanuel Wanna kulia akiwania mpira dhidi ya mlinzi wa timu ya soka ya Tigo FC, Maliki Halifa wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya timu hizo kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro ambapo zilitoka sare ya bao 2-2.
Juma Mtanda, Morogoro.
Timu ya soka ya kikosi cha Kupambana na Ujambazi FC, imenusurika kupokea kipigo kutoka kwa timu ya Tigo FC baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 katika mchezo mkali wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.
Mchezo huo ulikuwa na lengo la kuendeleza na kudumisha mahusiano kwa timu hizo hasa katika majukumu yao ya kazi mkoani hapa.
Juhudi za mshambuliaji wa timu ya Kupambana na Ujambazi FC, Mokili Lambo zilishindwa kuibeba timu hiyo licha ya kutengeneza pasi mbili zilizojaa mabao yaliyofungwa na Ramadhan Kapera (Pires) dakika ya 20 na Iddy Gamba katika dakika ya 37 na kujikuta wakipelekwa puta na wapinzani wao.
Timu ya Tigo ililazimika kutuliza akili baada ya kutandikwa bao hizo na kuanza kutengeneza mashambulizi makali langoni mwa wapinzani wao ambapo dakika ya 56, Daniel Charles alifunga bao la kwanza huku, Yunus Mansul akisawazisha bao la pili katika dakika ya 78 shuti lan umbali wa mita 20 na kujaa wavuni.
Kocha mkuu wa timu ya soka ya Tigo mkoa wa Morogoro, Seleman Kigwangalla akizungumza na MTANDA BLOG alisema kuwa baada ya timu ya soka ya Kupambana na Ujambazi FC inayomilikiwa na jeshi la polisi kuambualia sare, vijana wake walikosa umakini uliochangia kushindwa kuibuka na ushindi.
Kigwangalla alisema kuwa licha ya timu hiyo kuwa na nyota kama Clement Bazo na Mokili Lambo waliocheza ligi kuu Tanzania bara na Polisi Moro SC enzi hizo haikuwa tishio kwao na walifanikiwa kusawazisha bao hizo.
“Timu ya Kumbana na Ujambazi FC wana wachezaji wazuri kama Mokili Lambo na Clement Bazo lakini timu yetu ya Tigo ina wachezaji wazuri vijana na sare hii inatufanya tuombe mechi nyingine ya ya kirafiki na tunaimani tutaibuka na ushindi.”alisema Kigwangalla.
Kwa upande wa nahodha wa timu ya Kupamba na Ujambazi FC mkoa wa Morogoro, Hamis Mnunguye alisema kuwa lengo la mchezo huo wa kirafiki ni kudumisha umoja, upendo na kuendelezaa mahusiano baina ya taasisi hizo.
Mnunguye alisema kuwa michezo ni furaha na ina jenga afya bora lakini wao wametumia sehemu hiyo kama kubadilishana mawazo na kupeana mbinu za kuendelea kuwafichua waharifu ndani ya jamii zetu kupitia taasisi zao.
“Makampuni ya simu yana mchango mkubwa kwa kitengo chetu cha kupamba na ujambazi hasa kwa njia ya mitandao tumekuwa tukirikiana na kusaidia kukabiliana na wahalifu kwa njia hiyo”.alisema Mnunguye.
Kutokana na matokeo hayo timu hizo zinatarajia kurudiana tena kucheza mwingine wa kirafiki desemba 9 mwaka huu kwenye uwanja huo wa jamhuri mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment