Abraham Lincoln.
Na Geofrey Chambua
Tukubaliane kwamba maswali ni mengi sana kuliko majibu katika mambo haya. Kwa watakaofuatilia kwa karibu zaidi mambo yanayotendeka watagundua kuwa ukweli wa mambo ni tofauti sana na jinsi tunavyoambiwa na kutakiwa tuamini.
Duniani kuna mambo yanayotokea kwa bahati mbaya, lakini mengi tunayodhani ni ya bahati mbaya au ni kujirudia kwa historia ni mambo yaliyopangwa kutukia.
Na mengine yanaruhusiwa yatokee, kama ilivyo kwa tukio la Septemba 11, 2001, au matukio mengine mengi ya Septemba ambayo orodha yake haiwezi kutosha katika mada moja ya hapa
Huenda wasomaji wasikubaliane na hilo wakidai kuwa utafiti umepotoka, au umetegemea vyanzo visivyojitosheleza. Lakini tutazame lile tunaloweza kukubaliana, ambalo tunaweza kudai kuwa ni ama sadfa, bahati mbaya au kujirudia kwa historia juu ya Abraham Lincoln na John Kennedy.
Rais Lincoln alizaliwa Februari 12, 1809 na kufariki Aprili 15, 1865 akiwa na umri wa miaka 56. Rais Kennedy alizaliwa Mei 29, 1917 na kufariki dunia Novemba 22, 1963 akiwa na umri wa miaka 46.
Abraham Lincoln alichaguliwa kuingia katika Bunge la Marekani mwaka 1846 na John F. Kennedy naye alichaguliwa kuingia katika Bunge hilo mwaka 1946.
Hiyo ni tofauti ya miaka 100, au tuseme karne moja tangu kutokea kwa tukio moja hadi lingine. Pengine ni historia ilijirudia. Lakini kuna mengi zaidi ya hilo.
Mwaka 1856 Lincoln hakupata kura za kumtosha kupendekezwa kuwa mgombea Urais na mwaka 1956 Kennedy naye alishindwa kuteuliwa kugombea umakamu wa Rais 1956 hiyo ni miaka 100 barabara.
Abraham Lincoln alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 1860. John Kennedy akachaguliwa kuwa Rais 1960. Katika mbio za uchaguzi, Lincoln alimshinda Stephen Douglas aliyezaliwa mwaka 1813. Kennedy naye alimshinda Richard Nixon aliyezaliwa 1913.John Kennedy (pichani) na Abraham Lincoln, wote, kwa nyakati tofauti, walisoma sheria na wote waliwahi kufanya kazi jeshini.
Kennedy alichaguliwa kuwa Rais Novemba 8. Lincoln alichaguliwa kuwa Rais Novemba 8. Kennedy alikuwa mtoto wa pili katika familia yake. Lincoln naye alikuwa mtoto wa pili katika familia yake.
Wake zao Mary Todd Lincoln na Jacqueline Bouvier Kennedy walifiwa na watoto wakati waume zao wakiwa Ikulu. Mtoto wa Lincoln aliitwa Edward Baker Lincoln aliyefariki mwaka 1846 akiwa na umri wa miaka minne.
Katibu wa Abraham Lincoln aliitwa Kennedy, na katibu wa John Kennedy aliitwa Lincoln. Marais wote wawili waliuawa na watu waliotoka kusini mwa nchi hiyo, na wote, baada ya kuuawa, walirithiwa na watu waliotoka kusini mwa Marekani.
Marais wote wawili, Kennedy na Lincoln, walikuwa na Makamu wa Rais waliokuwa na majina ya Johnson. Makamu wa Rais wa Lincoln aliitwa Andrew Johnson ambaye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi mwaka 1847.
Makamu wa Rais wa Kennedy aliitwa Lyndon Johnson ambaye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi mwaka 1947.
Warithi wao wote (Makamu wao wa Rais) waliitwa Johnson. Andrew Johnson, ambaye alimrithi Lincoln, alizaliwa mwaka 1808. Lyndon Johnson, aliyemrithi Kennedy, alizaliwa mwaka 1908.
John Wilkes Booth, ambaye ndiye muuaji wa Lincoln, alizaliwa mwaka 1838. (si mwaka 1839 kama ilivyodaiwa na masimulizi fulani ya historia). Lee Harvey Oswald, ambaye alimuua Kennedy, alizaliwa mwaka 1939. Ni tofauti tu ya mwaka mmoja.
Wauaji wote wawili walijulikana kwa majina yao yote matatu, na majina yao kila mmoja yana herufi 15.
Wote wawili, Abraham Lincoln na John Kennedy, waliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Ijumaa na walipigwa risasi kichwani. Tofauti ni idadi tu ya risasi zilizopigwa
Lincoln alipigwa risasi akiwa katika ukumbi ulioitwa Ford kwa heshima ya aliyekuwa mtengenezaji maarufu wa magari duniani aliyeitwa Henry Ford.
John Kennedy alipigwa risasi akiwa katika gari lililoitwa "Lincoln" lililotengenezwa na kampuni ya Ford Motor Company iliyomilikiwa na Henry Ford.
Muuaji Booth, baada ya kumuua Lincoln, alikimbia kutoka ukumbini alimofanya mauaji na akakamatiwa katika bohari. Tofauti kidogo na huyo, muuaji Oswald alikimbia kutoka katika bohari na kukamatiwa ukumbini.
Wauaji wote wawili, Booth na Oswald, waliuawa kabla kesi dhidi yao hazijaanza.
Lincoln aliuawa mbele ya mkewe na Kennedy aliuawa mbele ya mkewe. Wake zao hawakudhurika wakati wa mauaji ya waume zao.
MAAJABU YA MARAIS HAWA WAWILI WOTE WALIKUFA SIKU YA IJUMAA KWA KUPIGWA RISASI KICHWANI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kimataifa /
kitaifa /
slider
/ MAAJABU YA MARAIS WAWILI WALIOFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA RISASI KICHWANI SIKU YA IJUMAA MAREKANI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment