Dar es Salaam. Mkazi wa Vingunguti kwa Kombo, Ally Hussein (34) amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh30,000 baada ya kupatikana na hatia ya kuchana karatasi 23 za uchaguzi wa wenyeviti wa Serikali za mitaa uliofanyika Desemba 21, 2014.
Hussein ambaye ni mfanyabiashara alihukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jana, kwa kuchana karatasi hizo kwa makusudi jambo lililosababisha kuvuruga uchaguzi, huku akijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Mshtakiwa alichana karatasi ambazo tayari zilikuwa zimeshapigiwa kura na wananchi katika uchaguzi wa kuwapata wenyeviti wa mitaa.
Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi, Adolf Sachore alisema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi wanane.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI SITA KWA KOSA LA KUCHANA KARATASI 23 ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MWENYEKITI WA MTAA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment