BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

TUNDU LISSU ASABABISHA WABUNGE WA UPINZANI KUTOKA NDANI YA BUNGE DODOMA


Wabunge wa upinzani watoka nje ya Bunge kupinga kukamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu.

Wabunge hao wametoka nje ya Bunge baada ya Naibu Spika kumtaka Mbunge wa Serengeti kutoka nje baada ya kutokea mabishano yaliyotokana na hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) ya kutaka Bunge lijadili swala Haki na Madaraka ya Bunge kukiukwa kwa wabunge kukamatwa ndani ya viwanja vya Bunge kinyume na utaratibu.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amewatoa nje ya Bunge, wabunge watatu wa CHADEMA, Halima Mdee (Kawe), Esther Bulaya (Bunda) na Marwa Ryoba (Serengeti).

Pamoja na hilo, baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi, Tundu Lissu amerejeshwa mahabusu hadi kesho (Leo) ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads