Marufuku ya Usafiri ya Trump: Marekani yataka kusimamishwa kwa muda.
Kurejeshwa tena kwa marufuku ya Rais Donald Trump kwa wahamiaji kutoka mataifa saba ya kiislamu, itasababisha "fujo tena", mawakili kutoka Marekani waonya.
Mawakili kutoka Washington na Minnesota, wanaiomba mahakama kuu ya nchi hiyo huko San Francisco kuendelea kuzuilia amri hiyo kuu kote nchini Marekani.
Wanaungwa mkono na kampuni za kiteknolojia, zinazosema kuwa marufuku ya usafiri inahujumu biashara zao. Mawakili wa utawala wa Trump, wanatarajia kujibu hilo baadaye Jumatatu. Rais wa Marekani Donald Trump katika jimbo lake la Mar-a-Lago huko Florida. Picha ya Februari 4, 2017
Amri ya kusimamishwa kwa muda ilitolewa siku ya Ijumaa, na jaji mmoja wa serikali huko Seattle, Jijini Washington, ya kuahirisha agizo hilo kuu la Bw Trump, ya kuwazuia miaji kutoka mataifa hayo saba yenye waislamu wengi.
Watu walio na visa kutoka Iraq, Syria, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen, itaendelea kukubaliwa Marekani hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa. Wakazi waishio Marekani kihalali kutoka mataifa saba yaliyotajwa wamekabiliwa na huzuni
Amri hiyo ya Jaji ilipokelewa kwa hasira na Bwana Trump, ambaye alidai kuwa usalama wa taifa umo hatarini.
Ombi la mahakama ya San Francisco tayari imepinga agizo la idara ya mahakama, kutekeleza kizuizi cha muda, kinachopangiwa kuzikubalia majimbo mawili kuwasilisha malalmishi yao inayosema kuwa marufuku hiyo ni kinyume na sheria na hatari kwa wakaazi wao, biashara na hata vyuo vikuu.
Mawakili wao wameiambia mahakama hiyo ya rufaa kuwa, marufuku ya aina yoyote, "itafufua madhara hayo, kutenganisha familia, kutatiza vyuo vyetu vikuu na hata mtaala, na pia kutatiza sekta ya usafiri".
Mawakili hao pia waliwasilisha taarifa za usalama wa taifa - inayowajumuisha mawaziri wa zamani wa kigeni John Kerry na Madeleine Albright, na pia mkurugenzi mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi (CIA) Leon Panetta - ambaye anaelezea marufuku hiyo ya usafiri kama isiyofaa, hatari na iliyojaa hasara tupu.BBC
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment