KIONGOZI MKUU WA UPINZANI AFUNGWA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA MAHAKAMANI
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, amepatikana na hatia ya ufujaji wa fedha na kupewa kifungo kilichohairishwa cha miaka mitano.
Hukumu hiyo inamzuia kuwania urais mwaka ujao dhidi ya Vladimir Putin.
Lakini bwana Navalny ameapa kuwania urais kwa vyovyote vile. Amekana mashtaka hayo na kusema kuwa atakata rufaa.
Kesi yake iliamuliwa baada ya kurudiwa kufuatia uamuzi wa mahakama ya haki ya ulaya, ambayo ilisema kuwa hukumu ya kwanza haikuwa ya haki.
Mkosoaji huyo mkubwa wa Rais Putin, alisema kuwa hukumu hiyo ambayo anadai ilichochewa kisiasa, ni ishara kuwa serikali ya Urusi inamtambua kuwa mtu hatari.
Bwana Navalny ,aliye na umri wa miaka 40 ambaye ni maarufu kutokana na kampeni yake dhidi ya ufisadi, ambayo iliwalenga maafisa wa vyeo vya juu walio karibu na serikali ya Urusi, anasema kuwa kesi hiyo ni ya kumzuia kutoka kwa mambo ya siasa.
0 comments:
Post a Comment