Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitafanya mazungumzo kusaka suluhu na mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa na kwamba, kipo tayari kwa lolote hata kama kitafutiwa usajili.
Dar es Salaam. Chama
cha Wananchi (CUF) kimesema hakitafanya mazungumzo kusaka suluhu na
mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na msajili wa
vyama vya siasa na kwamba, kipo tayari kwa lolote hata kama kitafutiwa
usajili.
Pia, chama hicho kimesema hakijuti kumkaribisha na
kumuunga mkono Edward Lowassa, ambaye aliteuliwa kugombea urais mwaka
2015 kwa tiketi ya Chadema na kuwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Maelezo hayo yalitolewa juzi na Naibu Mkurugenzi wa
Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande kujibu madai yaliyotolewa
na Profesa Lipumba alipohojiwa katika kipindi cha Funguka kinachorushwa
na kituo cha televisheni cha Azam.
Katika mahojiano hayo,
Profesa Lipumba alidai kuwa mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa sasa
hautamalizwa na mahakama pekee bali viongozi wa pande mbili na
kuzungumza, lakini Maharagande amesema haiwezekani kwa vile Lipumba
alishakwisha kukivuruga na hafai tena kuendelea kuwa kiongozi.
“Lipumba
anasema tukae tulimalize suala hili kwa kuongea sisi wenyewe. Jambo
hilo haliwezekani kwa kuwa kama kupandikiza chuki, uhasama, uharibifu wa
chama miongoni mwa wanachama na viongozi ameshafanya na kufanikiwa hilo
kwa baadhi ya wanachama na viongozi wake na kuharibu taswira ya chama
kwa jamii,” alisema Maharagande.MWANANCHI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment