DC ARUMERU AHUSISHWA KUTOA AMRI YA KUKAMATWA KWA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA
Arusha. Waandishi wa habari wawili jana walikamatwa na kuhojiwa katika Kituo cha Polisi cha Usa River mkoani Arusha, huku aliyetoa amri ya kukamatwa kwao akizua utata.
Wakati taarifa za awali zikidai ni amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, yeye alikana kuhusika na agizo hilo.
Waliokamatwa ni Bahati Chume mwandishi wa kujitegemea wa gazeti la Mwananchi Mkoa wa Kilimanjaro na Dorine Alois kutoka kituo cha Sunrise Radio cha jijini Arusha.
Waandishi hao walikamatwa walipokuwa wakifuatilia habari ya mgogoro kwenye machimbo ya kokoto katika Kijiji cha Kolila mpakani mwa wilaya za Arumeru na Hai.
Mnyeti alipoulizwa alikana kutoa amri hiyo akisema yeye hana ugomvi na waandishi wa habari.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment