BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DONALD TRUMP APATA PIGO BAADA YA MSHAURI WAKE KUJIUZULU

Afisa mkuu wa kampuni ya Uber Kalanick
Travis Kalanick, mkuu wa kampuni ya Uber amejiuzulu katika kundi linalomshauri rais Trump baada ya kukosolewa vibaya na wafanyikazi pamoja na Umma.

Bodi hiyo ambayo pia inamuorodhesha afisa mkuu wa kampuni ya Tesla Elon Musk inatarajiwa kukutana na rais siku ya Ijumaa.

Uber ni miongoni mwa kampuni za teknolojia zilizo na wasiwasi kuhusu athari za marufuku ya uhamiaji kwa nguvu kazi yake.

Kampuni hiyo imesema kuwa imeanzisha hazina ya dola milioni 3 kuwasaidia wale ambao wameathiriwa.

Watu hao ni pamoja na madereva wa Uber.

Hatahivyo Elon ametuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter akisema atahudhuria mkutano wa Ijumaa.

''Baraza la ushauri hutoa ushauri pekee na kuhudhuria kikao hicho hakumaanishi kwamba ninakubaliana na matendo yake'',alisema.

''Mimi na wengine tutapinga agizo la hivi karibuni la rais kuhusu uhamiaji na kutoa mapendekezo ya mabadiliko yatakayofanyiwa sera hiyo''.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: