KITENDO cha mama kumnyonyesha mtoto mdogo huku akiwa amekunywa pombe, kinatajwa kuwa ni hatari kwa afya.
Kitendo hicho kinatajwa kuwa ni hatari kwa sababu mtoto hunyonya kilevi
hicho kupitia maziwa ya mama yake na baadaye huathiri afya ya ubongo
wake.
Hayo yalisemwa na bingwa wa magonjwa ya akili wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dk. Plaxeda Swai wakati wa mahojiano na MTANZANIA
Jumapili mapema wiki hii.
“Unywaji pombe ni hatari kwa mjamzito na mama anayenyonyesha, mjamzito
haruhusiwi kutumia kilevi cha aina yoyote, pombe huathiri afya ya mtoto
aliyepo tumboni na anaweza akazaliwa akiwa na hitilafu kuanzia mfumo wa
fahamu, kuzaliwa na uzito mdogo, kichwa kidogo na madhara mengine
mengi.
“Wapo wanaofikiri kwamba madhara hujitokeza wakati wa ujauzito pekee na
wanapojifungua hawajali wakati wa kunyonyesha wanalewa, mama
anayenyonyesha akiwa amelewa, mtoto wake naye hulewa kwa sababu hupata
pombe kupitia maziwa ya mama yake.
“Hatua hiyo ni mbaya kwa afya ya mtoto, kwa sababu kilevi huenda
kuathiri afya ya ubongo wa mtoto na matokeo yake anaweza hata kupata
mtindio wa ubongo,” alisema Dk. Swai.
Alisema unywaji wa pombe kupita kiasi hasa zile zilizo kali, ni hatari
kwa afya ya mtumiaji kwa sababu anakuwa katika uwezekano mkubwa wa
kupata tatizo la kifafa baadaye katika maisha yake.
“Asilimia nne ya watu wanaokunywa pombe kali huishia kupata kifafa,
asilimia 50 hadi 75 ya watu wanaokunywa vilevi kupita kiasi huishia
kupata matatizo ya kiakili na asilimia 20 hadi 25 ya watu wenye matatizo
ya akili huwa wametumia aina moja au nyingine ya kilevi,” alisema Dk.
Swai.
Pia alishauri watu waliofikia hatua ya utegemezi wa vilevi na
wanahitaji kuondokana na hali hiyo ni vema wakawahi mapema kufika
hospitalini kwa matibabu.
“Tafiti zinaonyesha asilimia 80 ya watu ambao wamefikia kiwango cha
utegemezi wa pombe hupata tatizo la sonona na hofu iliyopitiliza,”
alisema.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ JE WAJUA !! MAMA KUMNYONYESHA MTOTO AKIWA AMELEWA, MTOTO HUNYONYA KILEVI ?
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment