JESHI LA POLISI MWANZA LAMDAKA MFANYABIASHARA WA MADAWA YA KULEVYA NA KETE 24O ZA HEROINE
Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mfanyabiashara wa vipuri vya magari aliyetajwa kwa jina moja la Ahmad (43) kwa tuhuma za kukutwa na kete 240 za dawa ya kulevya aina ya heroine.
Pia mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa Kanyerere, alikamatwa akiwa na dawa nyingine aina ya ndonga ambazo zilikuwa katika hatua za kufungwa kwenye kifaa maarufu cha kuhifadhia dawa hizo, jambo ambalo ni kosa la jinai.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi (pichani) alisema polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo akijihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kwamba waliendelea kufanya upelelezi dhidi ya tuhuma hizo.
“Polisi wakiendelea na upelelezi dhidi ya mtuhumiwa huyo, Februari 9 mwaka huu walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa ameingiza mzigo mkubwa wa dawa za kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kusambaza mtaani,”alisema Msangi.
Msangi alisema polisi waliizingira nyumba ya mtuhumiwa na walimuona akiendelea na shughuli yake ya kufunga dawa hizo katika kete ndogondogo maarufu kwa jina la pinchi.
“Baada ya mtuhumiwa kuona nje kuna maaskari alikimbiza mzigo huo chooni kupoteza ushahidi, hata hivyo polisi waliona kitendo hicho hivyo na kufanikiwa kuzikamata kabla ya kuchukuliwa na maji, huku askari wengine waliokuwa nje wakivunja bomba linalopitisha uchafu kwenda shimoni na kufanikiwa kupata ndonga mbili, Nyingine zikienda na maji,” alisema Msangi.Mwananchi
0 comments:
Post a Comment