BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KESI YA KUHAMASISHA MAANDAMANO YA UKUTA YAMHENYESHA MBUNGE GODBLESS LEMA ARUSHA


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema

Arusha.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imetupa pingamizi la mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema la kuitaka isisikilize kesi ya kuhamasisha maandamano ya Ukuta, bali kwanza ifikishwe Mahakama ya Katiba.

Lema, ambaye ni mbunge kupitia Chadema, anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kuhamasisha maandamano hayo ya chama chake yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka jana.

Mawakili wa Lema, John Mallya na Sheck Mfinanga, waliwasilisha ombi mahakamani hapo wiki iliyopita wakitaka kesi hiyo isikilizwe Mahakama ya Katiba kwa kuwa kuna hoja za kikatiba ambazo zitahitaji kutolewa maelezo na majaji watatu wa Mahakama hiyo.

Katika kesi hiyo, Lema anadaiwa kuhamasisha maandamano kwa njia ya mtandao wa kijamii (audio clip) aliyoitengeneza na kujirekodi ujumbe mfupi wa sauti na kisha kusambaza Agosti Mosi hadi 26, mwaka jana katika mitandao ya kijamii ya WhatsApp.

Hakimu Bernard Nganga alisema kosa alilofanya Lema siyo la kikatiba na hoja za kutaka kuhamishiwa shauri hilo Mahakama ya Katiba hazina mashiko kisheria.

Alisema sheria ipo wazi, kuwa mtu yeyote akihusika na kushawishi utendaji wa kosa hata kama halina madhara, muhusika ana makosa na adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili au kulipa faini. 


Hakimu Nganga alisema pingamizi za utetezi zimetupwa na shauri litaendelea kusikilizwa.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: