BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

NJIA KUU TANO ZA KUINGIZA MADAWA YA KULEVYA TANZANIA ZAFICHULIWA

WAKATI jiji la Dar es Salaam likitajwa kuwa kitovu cha kupitishia dawa za kulevya nchini, hatimaye njia tano zinazotumiwa na wafan- yabiashara ili kuziingiza nchini zimeanikwa.

Miongoni mwa njia ambazo wa- fanyabiashara huzitumia ni meli za mizigo ambazo husafirisha dawa kwa kutumia mapipa ambayo hu- ingizwa kwenye meli kwa kutumia boti.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Sa- laam, Paul Makonda, alitaja njia hizo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwendelezo wa mapambano ya vita dhidi ya dawa za kulevya, sam- bamba na kutaja majina ya vigogo 65 wanaotakiwa kuripoti Ijumaa Kituo Kikuu cha Polisi, kwa ajili ya kuhojiwa.

Kabla ya kutaja njia hizo alisema katika utafiti wake mdogo aliofan- ya, imegundulika sehemu ambayo ni rahisi kuingiza dawa za kulevya duniani kote ni Dar es Salaam.


Makonda alisema miongoni mwa njia ambazo wafanyabiashara huzitumia kuingiza biashara hizo Dar es Salaam ni meli.

“Watu wanaonunua dawa za kulevya Pakistan wakati meli ina- pakia mzigo, wao wanachukua boti wanachukua dawa za kulevya wa- nazipanga kwenye mifuko kama ya sukari, wanaweka kwenye mapipa na kufunga vizuri wanayaingiza kwenye meli,” alihadithia.

“Meli ikikaribia huku kwetu yako maeneo matatu wanatumia kutupa mapipa hayo ambayo ni Zanzibar, Bagamoyo na Tanga.

“Wanatupa mapipa baharini huku yakiwa yamefungwa GPS (Mfumo wa Utambuzi wa Maeneo) kisha meli inakwenda kutia nanga Bandari ya Dar es Salaam kushusha mzigo. 


“Baadaye timu iliyokubali- ana na watu hao, hutoka na boti kwenda eneo husika ambako mapipa yalitupwa huku boti hiyo ikiwa na mashine ya GPS ambayo uwezo wake ni kujua wapi mapipa yalipo, wanayaokoa mapipa wa- nayafumua, wanatoa dawa na kuzipaki vizuri tayari kuelekea Mtwara kisha Afrika kusini.”

Makonda alitaja njia nyingine kuwa ni ya magari. Alisema wa fanyabiashara ambao huenda nje kununua magari kwa ajili ya kuuza, wamekuwa wakitumia fursa hiyo kubeba dawa za kulevya.

“Mtu ananunua magari Japan lakini badala ya kuyaleta moja kwa moja Tanzania, ruti (njia) inakuwa ndefu. Anapita Bombay (Mumbai), India au Pakstan... wa- nafanya mambo yao ndipo wana- leta nchini,” alisema na kubainisha zaidi kuwa:

“Sehemu nyingine ni Marekani. Upo mchezo wa kufungua baadhi ya sehemu za magari na kuingiza dawa za kulevya.

“Ukichunguza Dar es Salaam wapo wenye maghala ya magari na wanauza bei ya chini, lakini si- jasema kuwa kila mwenye ghala la magari anayeuza kwa bei nafuu basi anauza dawa za kulevya.”

Makonda alitaja njia nyingine kuwa ni kupitia meli za mafuta.
“Kazi yetu ni kuangalia kiwango cha mafuta na vitu vilivyozingati- wa, kwa hiyo wanatumia udhaifu huo wanafanya yao.”

Pia alisema njia nyingine ni watu kuwa na maegesho ya boti zao, ku- chukua mzigo na kuuingiza kwenye maegesho na kuupakua kabla ya kuusafirisha.

Kadhalika, alisema njia nyingine ni kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaokwenda China kununua mzigo lakini wanajihusisha na usafirishaji wa watoto wa kike wenye umri wa kati ambao huwapa dawa za kulevya pamoja na dola za kimarekani 5,000 ili wasipate vikwanzo vya kuingia nchini humo.

Alisema ili mtu aingie China kwa sheria zao anatakiwa uwe na kianzio za dola za Marekani 5,000 (sawa na zaidi ya Sh. milioni 11).


Alisema yupo mama ambaye anajihusisha na biashara ya kuwasafirisha wasichana ambaye ana duka Sinza na Tanga na tayari wa- toto wawili wapo jela China.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads