BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MADIWANI WATIMUA WATUMISHI WANNE KWA UTORO KAZINI MBINGA


Picha ya maktaba aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu wa tatu mstari wa mbele kutoka kushoto katika picha ya pamoja na watumishi wa halmashauri ya Mbinga na madiwani.

Mbinga.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mbinga Vijijini limewafukuza kazi watumishi wanne na kumvua madaraka mtumishi mmoja.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya baraza kugeuka kamati na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ambrose Mtarazak amewataja waliofukuzwa kuwa ni Muda Ndunguru tabibu wa afya na muhudumu wa afya, Bapara Mwagombe wote kwa kosa la utoro.

Wengine ni Ofisa misitu msaidizi, Kevin Haule na ofisa utumishi Ally Kiasi waliotuhumiwa kwa kosa la kuingizia halmashauri hiyo hasara ya Sh46,680,000.

Pia baraza hilo limemvua madaraka ya ukuu wa idara mhandisi msaidizi wa ujenzi Kidongo Kisongo kwa kosa la uzembe kwa kushindwa kusimamia mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu.

Pia Baraza limewarudisha kazini watumishi watatu waliokuwa wamesimamishwa kazi ambao ni Ahsante Kuambano, Mratibu Tasaf, fundi sanifu, ujenzi Said Almas pamoja na Cosmas Masai ambaye ni mhasibu daraja la pili. Vilevile, limemfutia mashtaka afisa utumishi wa halmashauri hiyo, Emmanuel Kapinga.MWANANCHI
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment