BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASIKINI !! WETU SEPETU AENDELEA KUNG'ANG'ANIWA NA JESHI LA POLISI ISHU YA MADAWA YA KULEVYA.


Wema Sepetu.

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema bado linaendelea kumshikilia mwigi zaji wa filamu ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, na wenzake saba kuhusiana na dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini, Kamshina wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema bado wanaen- delea kumshikilia kwa kuwa wanasubiri majalada yake yafikishwe kwa Mwanasheria Mkuu wa Seri- kali ili kuyapitia na kuona ushahidi uliopo kisha sampuli kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

“Wema Sepetu na wenzake saba ambao walikamatwa na vielel- ezo na kwa kawaida majalada yao tumeyapeleka kwa wakili wa seri- kali ili ayapitie na kuona ushahidi uliopo pamoja na (kusubiri) kupata majibu kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,” alisema Kamishna Sirro.


“Kwa hiyo naamini upelelezi uki-kamilika watafikishwa mahakama- ni,” alisema bila ya kutaja muda.

Mama yake Wema, Miriam Sepe- tu alionekana katika Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana akiwa kwe- nye hali ya huzuni huku akisema anashindwa kujua kinachoendelea kituoni hapo.

Wakati huo huo, Kamshina Sirro alisema jeshi la polisi limewakama- ta watuhumiwa 84 wa dawa za kulevya na kete 18 za cocaine na heroine.

Sirro alisema watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo zilikamatwa baada ya kufanyika msako mkali katika kipindi cha siku mbili kuan- zia juzi.

Kamshina Sirro alisema oparesh- eni hiyo ni endelevu na kadri wana- vyowapata watuhumiwa wameku- wa wakiwasaidia kuwapatia taarifa na kuzifanyia kazi.

Aidha, Sirro alisema wanahitaji ushirikiano mkubwa na wenyeviti wa serikali za mitaa ili kuwapatia taarifa ya wale wanaojihusisha na dawa za kulevya lengo likiwa ni ku- tokomeza dawa hizo.

Kamishina Sirro awali alitangaza kushikiliwa na polisi kwa Wema Jumatatu akieleza kuwa ni mmoja wa watuhumiwa 112 ambapo 12 kati yao walikutwa wakiwa na vidhibiti vya kete za madawa ya kulevya.

Miongoni mwa waliokutwa na vidhibiti, alisema Kamishna Sirro, ni Wema ambaye upekuzi nyumbani kwake jijini uliibua misokoto ya bangi pamoja na rizla ambazo ni karatasi za kusokotea bangi.

Harakati za kuwakamata watu wanao- husika na dawa za kulevya katika jiji la Dar es Salaam kwa namna moja au nyingine ziliongezwa nguvu mwanzoni mwa wiki baada ya Rais John Magufuli kutaka zifua- tilie pia vigogo.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Sa- laam, Rais Magufuli alisema “Hakuna mtu maarufu, mwanasiasa, waziri au kiongozi yoyote au mtoto wa fulani, askari ambaye anajihusisha na dawa za kulenya asiachwe, hata awe mke wangu Janeth... kamata wote weka ndani.”

Alisema biashara ya dawa za kulevya kwa sasa nchini imefikia katika hali mbaya na kwamba zinauzwa kama njugu nchini.

Alitaka vyombo vyote vya ulinzi vinavy- oendelea kupambana na dawa za kulevya viendelee na mapambano.

Alisema biashara ya dawa za kulenya kwa sasa nchini inapoteza nguvu kazi za Watanzania wengi haswa vijana, na kwam- ba vyombo vyote vya ulinzi vinapaswa kushirikiana ili kuwakamata.

Rais Magufuli aliwataka wahusika kuu- winda mtandao wote unaojihusisha na bi- ashara ya dawa za kulevya.

“Haiwezekani wauzaji wapo mtaani wanatanua tu, hawakamatwi,” alisema Rais Magufuli.


“Kwa mfano kuna muuzaji mkubwa yuko mkoani Lindi, alishikwa na dawa za kulevya lakini sijasikia hata siku moja akitangulizwa Mahakamani.Ninajua kuna viongozi wanamtetea,” aliongeza.

Rais Magufuli alikuwa akimzungumzia mtu anayeaminika kuwa ‘mzungu wa unga’ aliyekuwa akitafutwa zaidi nchini.

Ali Khatibu Haji (47), maarufu kwa jina la Shikuba, alikamtwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ( JNIA) Machi, 2014 baada ya kuwindwa kwa miaka miwili kabla ya kuhamishiwa mkoani Lindi. 


Anatuhumiwa kuwa kiongozi wa genge lenye makao yake Afrika Mashariki lakini likiwa na uhusiano wa kibiashara mpaka China, Brazil, Canada, Japan, Marekani na Uingereza.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment