Picha ya maktaba bwana na bibi harusi wakiwa ndani ya maji wakati wa hafla yao ya kufunga ndoa.
Arusha. Maharusi Munisi Roy (25) na Nembrice Munyaga (20) waliofariki kutokana na mafuriko Februari 24, wanatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Ilkisongo Kata ya Sambasha wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Maharusi hao, walifariki juzi baada ya kuzolewa na mafuriko wakiwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Premio, pamoja na ndugu wengine watatu. Diwani wa kata ya Sambasha, Roy Sabaya amesema marehemu hao watazikwa baada ya kukamilika taratibu za mazishi.

0 comments:
Post a Comment