BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MRATIBU WA TASAF ASIMAMISHWA KAZI KWA KUSAJILI KAYA HEWA 28


Mkalama. Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida, limemsimamisha kazi kwa muda usiojulikana mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Athumani Dulle, kwa tuhuma za kusajili kaya 28 zisizokuwa na sifa.

Bila kutajwa kiasi kilichotumika kulipa kaya hizo, Dulle amesimamishwa kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazomkabili.

Pia wa kikao kilichopitisha uamuzi huo, James Mkwega amesema kikao hicho kimewafukuza kazi watumishi watatu wa halmashauri huyo, na kumsimamisha mmoja kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo utoro kazini.

Watumishi hao walioadhibiwa kwa utoro kazini kuwa ni James Kidumo Moses (Ofisa Mifugo Msaidizi), Sera Ogoti (Ofisa Muuguzi), Seleman Ntunga (Fundi Sanifu Maabara).Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: