BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKE WA MLANGUZI MKUU WA MADAWA YA KULEVYA AKATAZWA KUMUONA MUMEWE GEREZANI

Mlanguzi mkuu wa madawa ya kulevya, raia wa Mexico, Joaquin Guzman, amelalamika alipofikishwa mahakamani mjini New York, akisema kuwa anazuiliwa kwa njia isiyofaa katika gereza moja la Marekani.

Guzman, ambaye amefanikiwa kutoroka mara mbili kutoka magereza ya Mexico, aliwahi kutoroka kupitia kikapu kikubwa na mara ya pili alichimba shimo kubwa chini ya ardhi kupitia seli yake. Hivi sasa anazuiliwa akiwa pekee katika gereza lenye ulinzi mkali jijini New York.

Mawakili wake wanasema kuwa mkewe amezuiliwa kumtembelea tangu asafirishwe chini ya ulinzi mkali kutoka Mexico mwezi uliopita. Mkewe El Chapo Guzman

Wakati mwingi Guzman haruhusiwi kutangamana na wafungwa wengine.

Guzman anashtakiwa kwa kuwa na silaha kinyume cha sheria ya ulagunzi wa madawa ya kulevya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: