BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAFUNZI WA SEKONDARI AKAMATWA AKIUZA MADAWA YA KULEVYA MBEYAMbeya. Vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda imetua jijini hapa baada ya polisi kutangaza kumkamata mwanafunzi anayesoma sekondari akiwa na kete 24 za cocaine eneo la Mbalizi.

Kamanda wa polisi mkoa, Dhahir Kidavashari amesema leo kuwa polisi wamemkamata mwanafunzi huyo akiwa anaziuza dawa hizo kwa watu mbalimbali na kwamba upelelezi wa kuwadaka mapapa unaendelea.

Kukamatwa kwa kijana huyo kunatokea siku moja baada ya Rais John Magufuli kuunga mkono kazi ya Makonda huku akiwaagiza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wote wanaojihusisha na dawa za kulevya bila kujali huyu ni nani.


Kidavashari amesema kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya ilikuwa ikiendelea, lakini sasa imepata msukumo mpya ambao unalenga kuukata mnyororo mzima wa mtandao unasambaza dawa hizo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment