BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHAMA CHA WANANCHI CUF CHAMFUKUZA UANACHAMA MBUNGE MKANYAGEN ZANZIBAR


MOHAMED HABIBU MNYAA


THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF –Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA
Imetolewa leo Tarehe 7/2/2017

Leo tarehe 7/2/2017 Mkutano Mkuu wa Tawi la Chanjaani, Jimbo la Mkoani wilaya ya Mkoani-Pemba, umefanya maamuzi ya kumfukuza uanachama wa CUF Mohamed Habibu Mnyaa kutokana na kukiuka katiba ya chama Ibara ya 12 (6)(7)(16).


Kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa wa kuwagawa wanachama, kueneza taarifa za upotoshaji dhidi ya viongozi na Chama, kufanya vitendo vya hujuma za kutaka kukidhoofisha Chama, kudharau na kushindwa kuhudhuria na kutoa ushirikiano kwa tawi lake kila alipotakiwa kufanya hivyo. 

Mkutano Mkuu wetu wa leo umehudhuriwa na wajumbe halali 112 kati ya wajumbe wote halali 113. Wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix) kuhusu wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;

“Kumchukulia hatua za nidhamu mwanachama au kiongozi yeyote wa tawi hilo, ikiwa ni pamoja na kumpa onyo, karipio, karipio kali, kumsimamisha uanachama au uongozi wa Chama kwa muda, na hata kumuachisha au kumfukuza uanachama wa Chama”

Mohamed Habibu Mnyaa alijiunga na CUF katika tawi hilo tarehe 28 septemba mwaka 1999 na kukabidhiwa kadi yenye Namba ya usajili 029033. 


Mohamed ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni kwa muda wa vipindi viwili 2005-2015, amekuwa na mwenendo huo mbaya na usiofaa kwa Chama na viongozi wake tangu alipokosa ridhaa ya wanachama na Maamuzi ya vikao vya Chama kumpitisha kugombea kwa mara nyingine tena katika nafasi ya ubunge mwezi August, mwaka 2015. 

Mohamed amefukuzwa uachachama akiwa ni mwanachama wa kawaida wa tawi la Chanjaani asiyekuwa na wadhifa wowote mwingine ndani ya Chama.

Kwa mujibu wa Katiba ya CUF ibara ya 108(5) kuhusu Nidhamu ya chama na Muda wa kukata Rufaa inaeleza kuwa;

“Mwanachama au kiongozi yeyote aliyeamua kukata Rufaa kwa jambo lolote lile, basi atafanya hivyo kwa ngazi iliyo juu ya kikao kilichotoa maamuzi ambayo hakuridhika nayo katika kipindi kisichozidi siku kumi na nne (14) tokea siku uliotolewa uamuzi huo” ni hiyari yake kuona kama inafaa kukitumia kifungu hiki au kutokitumia."

Tunatoa wito kwa wanachama wote wa tawi la Chanjaani, kuzingatia wajibu wao wa kikatiba na kuheshimu taratibu, kanuni na kulinda nidhamu na heshima ya Chama chetu ndani ya Chama na ndani ya jamii kwa ujumla. 


Uongozi wa tawi hautasita kutekeleza matakwa ya katiba pale itakapobainika kwa mwanachama yeyote kwenda kinyume na maamuzi na misimamo ya Chama.

HAKI SAWA KWA WOTE
KOMBO MOHAMED MAALIM
KATIBU WA TAWI LA CHANJAANI, JIMBO LA MKOANI-PEMBA
Mawasiliano: 077 815 3414
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: