BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO SC, KMC FC WATANGAZA VITA LIGI DARAJA LA KWANZA 2016/2017

Mshambuliaji wa Polisi Moro sc, Salum Kihimbwa (Chuji) akimiliki mpira dhidi ya mlizni wa KMC FC ya Dar es Salaam, Erick Mawala wakati wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara katika uwanja wa jamhuri Morogoro na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Juma Mtanda, Morogoro.

Wakati ligi daraja la kwanza Tanzania bara msimu wa 2016/2017 ikielekea ukingoni, klabu ya Lipuli FC ya Iringa imerejea ligi kuu Tanzania bara msimu ujao baada ya kufanya vizuri katika kundi A kwa kuibuka kinara kwa pointi 29.

Katika kundi C, Singida United FC ipo katika matumaini makubwa ya kuibuka kidedea katika kundi hilo kwa kukusanya pointi 26 huku Alliance Academy ikivuna pointi 25 ambapo mchezo wa mwisho utaamua timu ipi itacheza ligi kuu.


Endapo mchezo wa mwisho kati ya Alliance Academy na Singida United ukimalizika kwa sare ya yoyote itakuwa na manufaa kwa Singida United lakini Endapo Alliance Academy itashinda ndio itayotinga ligi kuu.

Wakati upinzani huo ukijitokeza kundi C, upinzani mwingine umejitokeza katika kundi B baada ya klabu ya Polisi Moro SC kuongoza kwa idadi ya bao moja dhidi ya KMC FC ya Dar es Salaam.

Polisi Moro SC na KMC FC zina piniti sawa 17 kila mmoja wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa huku mabenchi yao ya ufundi yakikuna vichwa kuhakikisha mmoja wao anatinga ligi kuu msimu ujao.

Katika mchezo kati ya vinara wa kundi B, Polisi Moro SC dhidi ya KMC FC ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku mwamuzi wa kati na msaidizi namba moja wakitupiwa lawama kwa kushindwa kumudu mchezo huo na kuzua kelele kutoka kwa mashabiki.

Mwamuzi wa kati katika mchezo huo wa Polisi Moro SC na KMC FC, Daniel Warioba alilalamikiwa na msaidizi wake huyo na mashabiki wa soka katika uwanja wa jamhuri Morogoro baada ya kipindi cha kwanza kuchezesha dakika 50 huku dakika ya 88 msaidizi huyo akishindwa kuelewana na mwamuzi wake wa kati.


Mchezo huo ulishuhudiwa na MTANDA BLOG huku kukiwa na upinza mkali ambapo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika dakika ya 88, nje ya 18 ya lango la Polisi Moro kulitokea madhambi na mchezaji kuumia na mwamuzi kupuliza kipenga cha kosa na kuita huduma ya kwanza lakini wakati mchezaji anapatiwa huduma ya kwanza msaidizi wake, Makore Marandi tayari aliashiria adhabu hiyo kuwa ni penalti.

Hali ya kujichanganya kwa msaidizi huo kulitokana na mbinu za udanganyifu za wachezaji wa KMC FC waliochukua mpira na kwenda kuuweka katika boksi la penalti eneo la Polisi Moro lakini baada ya mchezaji kutibiwa, mwamuzi wa kati alirejesha adhabu kupigwa nje ya 18.

Polisi Moro SC ndio walionza kupata bao kupitia kiungo, Fred Tangalu kwa mpira wa adhabu ndogo nje ya 18 baada ya kufumua shuti kali na mpira kujaa wavuni dakika ya 24 huku KMC FC wakisawazisha bao lao dakika ya 69 kwa kichwa kupitia kwa Joseph John akiunganisha mpira wa adhabu uliotokea nje ya 18 lango la Polisi Moro.

Kutokana na matokeo hayo ya sare ya bao 1-1, kundi hilo sasa litasubiri kumpata mbabe katika michezo yao ya mwisho kwa Polisi Moro endapo atapata matokeo mazuri huku akiombea dua mbaya kwa KMC FC ipoteze mchezo wao dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Kibarua hicho sio rahisi kwa Polisi Moro au KMC FC kwa kuombeana dua mbaya katika michezo yao ya mwisho lakini Njombe Mji FC yenyewe ina pointi pointi 16 huku ibakiwa na michezo miwili kibindoni na endapo itashinda yote itakuwa na poiniti 22 na kuwa kinara katika kundi hilo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: