RAIS ATANGAZA UKAME KUWA JANGA LA KITAIFA BAADA YA VIJIJI VINGI KUKUMBWA NA BAA LA NJAA.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza ukame kuwa janga la kitaifa.
Hiyo inafuatia ukame uliokithiri nchini humo kwa zaidi ya nusu mwaka, huku majimbo 23 kati ya 47 ya nchi hiyo kukumbwa na baa la njaa.
Kumeshuhudiwa uhaba mkubwa wa chakula hasa katika maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo ambayo yameshuhudia ukosefu wa mvua huku wanyama na raia wakifa.
Rais Kenyatta amewaonya watu wanaosambaza chakula cha misaada kutouza chakula hicho na "kujitajirisha", Taarifa ya Rais ilisema.
"Sitamvumilia mtu yeyote ambaye atajaribu kuchukua fursa hii na kula pesa za umma."
Naomba sote tuyachunguze mashirika likiwemo tume ya kupambana na ufisadi (EACC) kuwa katika mstari wa mbele kukabiliana na wafisadi wakati wote wa usambazaji chakula cha msaada. Sitaki serikali ilaumiwa kwa kuchukua nafasi hii eti inawapunja raia." Uhuru Kenyatta alisema.
Onyo hilo linatukia wakati ambapo shirika la kimataifa la msalaba mwekundi na lile la Red Crescent, zikionya kuwa Zaidi ya watu milioni 11 kutoka Kenya, Ethiopia na Somalia wamo katika hatari ya kufa njaa na wanahitaji kwa haraka msaada wa kibinadamu, kutokana na kukithiri kwa ukame.
Nchini Ethiopia, ukame mmbaya kwa zaidi ya karne moja ulikithiri nchini humo, kwa pamoja na mmiminiko wa watu waliokimbia vita nchini Somalia, shirika la msalaba mwekundu umeonya.
Aidha, shirika hilo linaongeza kuwa, vyanzo vya maji nchini Kenya, vimekauka, na kusababisha kuangamia kwa idadi kubwa ya mifugo.
Bw Kenyatta amesema kuwa, kiangazi hicho kikali, kinawaathiri pia wanyama pori
0 comments:
Post a Comment