TANZANIA YAILAZIMISHA UJERUMANI KULIPA FIDIA KWA MAOVU WALIYOYAFANYA KARNE ILIYOPITA
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Konchanke
Afisa wa ngazi ya juu wa Tanzania amesema serikali inazingatia uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria kulilazimisha koloni la zamani-Ujerumani ilipe fidia kwa maovu yaliyofanywa karne moja iliyopita.
Waziri wa ulinzi Hussein Mwinyi amewaambia wabunge hii leo kwamba serikali ya Tanzania inataka walipwe fidia maelfu ya watu wanaosemekana walidhalilishwa, waliteswa na kuuliwa na vikosi vya Ujerumani walipokuwa wakiuvunja nguvu uasi wa kikabila.
Ujerumani iliitawala Tanganyika ya zamani kati ya mwaka 1890 hadi 1919. Pindi Tanzania ikishinikiza kulipwa fidia basi nchi hiyo ya Afrika Mashariki itakuwa inafuata mfano wa hivi karibuni wa Kenya ambako kundi la wazee walishinda kesi dhidi ya serikali ya Uingereza kwa madai ya mateso yaliyofanywa na maafisa wakati wa ukoloni.
Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania haukusema lolote hadi sasa kuhusu madai hayo. Je, unadhani Ujerumani inapaswa kulipa fidia hiyo ijapokuwa wanatoa misaada ya kimaendeleo nchini? DW (Kiswahili)
0 comments:
Post a Comment