Jamii mpya ya mjusi aliyetambuliwa hivi majuzi, ambaye ana tabia ya kujibambua magamba yake mwilini mwake na kumuacha adui anayetaka kumla, pindi anaposhambuliwa.
Jamii nyingi za mijusi hukata mkia, wanaposhambuliwa, lakini mjusi huyu aliye na magamba kama samaki, ana magamba mengi mno yanayobambuka kwa urahisi.
Mjusi huyu aliyetambuliwa, ni bingwa wa usanii, wanasema wanasayansi, wakiwa na kiwango kikubwa mno cha magamba kuliko aina yoyote ya mjusi duniani.
Ngozi ya mjusi huyo inayofanana na magamba ya samaki, ina mtindo wa kukatika katika.
Anaponaswa na adui, mjusi huyu mwenye magamba kama samaki, hapotezi tu magamba pia hata na ngozi yake
Sehemu kubwa ya magamba hayo yameshikanishwa na eneo dogo mno mwilini mwa mnyama huyo na kuwa rahisi kubambuka.
Aidha, ndani ya magamba hayo kwenye ngozi, kuna maeneo ya kukatika katika.
Hata ingawa jamii nyingi ya mijusi, hawawezi kupoteza ngozi zao kwa urahisi hadi pale wakabwe kwa nguvu, mjusi huyu ana uwezo huo haraka anapoguswa
Ajabu ni kwamba, ngozi na magamba mengine humea kwa kasi sana, kwa kipindi cha wiki chache tu.
Jamii hiyo ya mujusi imegunduliwa katika maeneo ya mapango ya Tsingy, kaskazini mwa Madagascar.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment