BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

THE MIGHT ELEPHANT YAKUBALI KIPIGO KUTOKA KWA MAWENZI MARKET LIGI DARAJA LA PILI MORO

Mshambuliaji wa The Might Elephant ya Songea, Japhet Gama akiwania mpira na kiungo wa Mawenzi Market FC, Marthin Mdime kulia wakati wa ligi daraja la pili Tanzania bara katika mchezo uliofanyikwa uwanja wa jamhuri Morogoro na The Might Elephat kuambulia kipigo cha bao 2-0.

Juma Mtanda, Morogoro

Timu ya soka ya Mawenzi Market FC sio timu ya mchezo mchezo, ndivyo unavyoweza kusema hivyo kufuatia kuihenyesha na kuwapigisha kwata maafande wa The Might Elephant FC ya Songea katika ligi daraja la pili Tanzania bara kisha kuitandika bao 2-0 katika mchezo mkali uliopigwa uwanja wa jamhuri Morogoro.

The Might Elephant FC ilijikuta kwenye wakati mgumu kwa kushindwa kuhimili kasi ya wachezaji wa Mawenzi Market FC na kupelekea kutoa mwanya wa kushambuliwa mara kwa mara na kufungwa mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza.

Mshambuliaji Hamis Mkopi ndiye aliyeonekana hatari zaidi katika mchezo huo baada ya kufunga mabao yote mawili katika dakika ya 15 na 43.

Mkopi alikuwa msumbufu katika mchezo huo ambapo alianza kufunga bao lake la kwanza kwa kunasa mpira wa krosi uliochongwa na, Mohamed Makalanga ambapo kabla ya kufunga bao hilo mpira huo ulimgonga mlinzi wa The Might Elephant FC, Rashid Hamis na kushindwa kuondoa eneo la hatari kabla ya kumkuta mfungaji akiwa ndani ya sita na kufyatua kombora kali na kujaa wavuni.

Bao la pili alifunga kwa kupokea pasi ya, Twalib Hassan kisha kumlamba chenga mlinzi huyo huyo na kupachika bao la pili mbele ya kipa tegemeo, Ahamadi Mwinyihaji.

Kutokana na ushindi huo Mawenzi Market FC ndiyo inaongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi 17 huku The Might Elephant wakibakia na pointi zao 14 wakati Namungo Fc ikiwa na pointi 13 kufuatia kulazimisha sare na Mkamba Rangers.

Kocha mkuu wa timu ya The Might Elephant, Francis Samatta alieleza kufurahishwa kwake na matokeo ya mchezo huo licha ya kupoteza lakini akimpongeza maamuzi wa kati wa mchezo huo, Mgao Masaoanga kutoka Lindi kwa kuchezesha mchezo kwa kufuata sheria 17.

“Tumepoteza mchezo huu lakini bado tupo katika mbio za kusaka nafasi ya kwanza lakini Mawenzi Fc walistahili kushinda japo sisi bahati haikuwa yetu kwani tumepoteza nafasi za wazi za kufunga lakini mwamuzi amechezesha mchezo wetu bila upendeleo wowote sio kwa wenyeji wala wageni.”alisema Samatta.

Samatta alisema kuwa timu yake bado ipo katika mbio za kupanda ligi daraja la kwanza na wanajipa upya kwa michezo yao iliyobakia.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment