UZEMBE, DHARAU CHANZO CHA YANGA KUTANDIKWA 2-1 NA SIMBA
Kocha msadizi wa Yanga, Juma Mwambusi
Kocha msadizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema uzembe wa wachezaji wake ndiyo ulioigharimu timu yake kufungwa.
Alikiri kusema kuwa kadi nyekundu aliyopewa beki wa Simba, Janvier Bokungu ndiyo iliyoimaliza timu yake kwani Simba walikuja na nguvu ya ajabu na kupata mabao.
Amesema kuwa hawakuwa vizuri katika umaliziaji na hata ukabaji, mabeki waliwasindikiza wachezaji wa Simba kwa macho na kuwafanya kufika kirahisi golini kwetu mara nyingi kipindi cha pili.
Mwambusi pia amesema kuumia kwa Thaban Kamusoko kulisababisha pengo kwani hata mchezaji aliyeingia, Said Juma Makapu hakuwa katika kiwango cha mchezo licha ya kuwa ni mchezaji wetu.
"Simba walikuwa vizuri katikati kwa sababu waliweka watu wengi, watu tuliowapa majukumu ya kusaidia katikati hawakufanya kazi yao kwa haraka na ndiyo maana alipoumia Kamusoko tulimuingiza Said Makapu, ambaye ni kijana na hakuweza kutimiza majukumu vizuri kama ilivyokuwa kwa Kamusoko," alisema Mwambusi.
"Baada ya Simba kuwa pungufu walikuja kwa kasi na kujitoa kwa sababu hawakuwa na cha kupoteza na walitushinda kwa sababu sisi tulipooza na kusahau kuwa bado tuko uwanjani na tunahitaji mabao zaidi." MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment