BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALIOFUKUZWA MSUMBIJI WAMEFUKUZWA KIHALALI

Watanzania wanaorudi kutoka Msumbiji wakiwa katika Kijiji cha Kilambo mkoani Mtwara baada ya kushuka katika kivuko cha MV Kilambo kinachofanya safari zake kati ya mpaka wa Tanzania na Msumbiji. Picha na Haika Kimaro

Dar es Salaam.
Serikali imesema wananchi waliofukuzwa Msumbiji wamefukuzwa kihalali kwa sababu hawakufuata taratibu za uhamiaji na wengine walijihusisha na vitendo vya kihalifu wakiwa ugenini.

Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga amesema operesheni inayofanyika Msumbiji iliwahi kufanyika pia hapa nchini ikiwa na lengo zuri la kuwaondoa wahamiaji haramu. 


Hata hivyo, Dk Mahiga amesema Serikali ya Tanzania na Msumbiji zinaendelea na mazungumzo kuhakikisha kwamba Watanzania hao wanakuwa salama wakati operesheni hiyo ikitekelezwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: