BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WEMA SEPETU AHAMIA CHADEMA

Msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu akiwa kwenye vazi la chama cha mapinduzi (CCM)


Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kunatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwamo msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28).

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.

Msanii huyo ambaye alishinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: