BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Makonda ahutubia mbele ya Rais Mgufuli, asifu vita ya dawa za kulevya

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amehutubia wakati wa uzinduzi wa barabara za juu, Ubungo na kujisifu kuwa vita ya dawa za kulevya imesaidia vijana zaidi ya 11,000 kuacha matumizi ya dawa hizo.

Makonda pia alisema amekabidhi miradi 20 ya maji Dawasco na kuwa miradi mingine itapunguza tatizo la maji kwa asilimia 90.

“Inawezekana kabisa asiwepo mtu anayekuunga mkono, lakini ipo siku Mungu atakuuliza Tanzania aliyokupa umeifanyia nini,”alisema Makonda na kupigiwa makofi

Makonda alizungumza mara baada ya Rais John Magufuli, kuwasili Ubungo akiwa na gari la mwendokasi. 


Rais aliambatana na Rais wa Benki ya Dunia, jim Yong Kim. Rais Magufuli amezindua ujenzi wa barabara za juu, katika eneo hilo la Ubungo.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: