BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TANZANIA NI MOJA YA NCHI AMBAZO RAIA WAKE HAWANA FURAHA KABISA DUNIANI

Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani.

Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155.

Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo ichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inaangazia furaha watu waliyo nayona ni kwa nini


Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani


Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya katika ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani. 

Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.

Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini. 


Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147 mtawalia.BBC

Nchi zenye watu walio na furaha na wasio na furaha Duniani
Nchi zenye watu walio na furaha Duniani Nchi zenye watu wasio na furaha Duniani
1. Norway 146. Yemen
2. Denmark 147. Sudan Kusini
3. Iceland 148. Liberia
4. Uswizi 149. Guinea
5. Finland 150. Togo
6. Uholanzi 151. Rwanda
7. Canada 152. Syria
8. New Zealand 153. Tanzania
9. Australia 154. Burundi
10. Sweden 155. Jamhuri ya Afrika ya Kati 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: