
Tarehe 3 Septemba mwaka 2012, afisa huyo wa polisi aligongwa na gari la kifahari aina ya Ferrari lilokuwa likiendeshwa na bwana Vorayuth.
Majaribio kadha ya utawala wa Thailand kumfikisha Vorayuth mbele ya sheria, yanaonekana kuwa mvutano na familia tajiri nchini humo.
Ukweli kuhusu kuuawa kwa polisi uko wazi.

Kwa zaidi ya miaka minne Vorayuth Yoovidhaya hajafika mahakamani.
Polisi Wichian Klanprasert alikuwa akiendesha pikipiki yake mjini Bangkok, wakati aligongwa na gari aina ya Ferrari, ambayo iliuvuta mwili wake umbali wa zaidi ya mita 100 barabarani.
Maafisa wa kuchunguza waliyafuata matone ya mafuta ya breki hadi jumba la kifahari la familia hiyo tajiri lililo umbali ya kilomita moja hivi.
Gari hilo la Ferrari lililokuwa limeharibiwa vibaya, lilikuwa hapo na polisi wamamkama dereva aliyekuwa ameajiriwa na familia kama mshukiwa mkuu.
Wakati polisi waligundua kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na bwana Vorayuth, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 27, alifanyiwa uchunguzi na kupatikana akiwa na kiwango kikubwa cha pombe kwenye damu
Tangua mwaka 2013 bwana Vorayuth amekataa kufika mara saba mbele ya mahakama, huku mawakili wakitoa sababu kadha zikiwemo kuwa yuko ziara za kibiashara nje ya nchi au anaumwa.
Lakini picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa na marafiki zake, zanaonyesha kuwa mara kadha amekuwa nchini Thailand na pia yeye husafiri kote duniani kushiriki mashindano ya uendeshaji magari kwa kasi na kustarehe.BBC
0 comments:
Post a Comment