BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

EDWARD LOWASSA AELEZA KISA KILICHOMPONZA HADI KUITWA NA KUHOJIWA POLISI DAR ES SALAAM

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mwanachama wa Chama cha Chadema Edward Lowassa, amehojiwa na kuondoka katika Ofisi ya mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai baada ya kutakiwa kufika katika Ofisi hiyo siku ya Jumatatu kwa sababu zisizojulikana .

Kulingana na gazeti la The Citizen, Lowassa ambaye alitakiwa kuwasili katika Ofisi ya DCIO muda wa saa nne aliwasili saa tatu na dakika 58 asubuhi.

Msafara wake ulikuwa na magari sita ikiwemo magari mawaili ya polisi yaliokuwa na polisi waliojihami .

The Citizen linasema kuwa usalama ulikuwa umeimarishwa katika barabara ya Ohio.

Waandishi habari walikatazwa kuchukua picha za Lowassa.

Katika mahojiano ya simu na gazeti la The Citizen, alisema kuwa anashuku kwamba agizo hilo la kutakiwa kujiwasilisha linatokana na matamshi aliyotoa mjini Dar es salaam siku ya Ijumaa wakati wa hotuba ya Iftar.

Wakati wa hotuba hiyo, alimtaka rais Magufuli kuwaachilia huru wahubiri wa Kiislamu ambao walikuwa wamekamatwa kwa zaidi ya miaka minne bila kesi zao kuamuliwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: