BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI ABDULLAZIZ ABOOD AWAPIGIA MAGOTI WAZAIDIZI WA KISHERIA

 

Na John Nditi, Morogoro.
WASAIDIZI wa kisheria nchini wametakiwa kujenga uaminifu mkubwa kwa jamii na kuwasaidia walengwa katika kupata haki zao ndani ya familia na kwa jamii kiujumla.

Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood alisema hayo hivi karibuni mjini hapa wakati akizindua mradi wa kuongeza wigo wa kupata haki kwa wote hasa kwa wanawake. 


Mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria na unaotekelezwa na mtandao wa Wasaidizi wa Kisheria Tanzania (Tapanet) kwa ufadhili wa Legal Service Facility (LSF).

Alisema, serikali kupitia bunge lake inawatambua wasaidizi wa kisheria na kuwadhamini ndio maana limepitisha sheria ya kuwatambua na kutambua michango yao katika jamii. Mbunge huyo alisema, hivi sasa sheria hizo zinatungiwa kanuni ili zitumike kuwaongoza kufanya kazi kwa kufuata utaratibu unaotakiwa.


Abood alisema, serikali kupitia bunge inawatambua wasaidizi wa kisheria na kuwadhamini ndio maana walipitisha sheria ya kutambua michango yao katika jamii na hivi sasa sheria hizo zinatungiwa kanuni ili zitumike kuwaongoza kufanya kazi kwa kufuata utaratibu.

Naye Msaidizi wa Kisheria, Bonny Matto alisema migogoro mingi ya ardhi katika jamii inachangiwa na mabaraza ya ardhi ya kata na watendaji wa vijiji kutokuwa na elimu ya kutosha katika kutatua migogoro hiyo. 


Alisema kuwa baadhi yao wanaitumia migogoro hiyo kama njia ya kujipatia kipato kutokana kutolipwa mshahara, ukosefu wa elimu ya kutosha katika kusaidia jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Tapanet, Cosma Bulu alisema wasaidizi wa kisheria wanafanya kazi za kujitolea, hivyo serikali iangalie jinsi ya kuwasaidia waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi. 


Hata hivyo aliiomba serikali wakati wa kupanga bajeti ya majimbo wafikirie kuweka bajeti ya wasaidizi wa kisheria iwasaidia wakati wa kutoa huduma ndani ya jamii. 

Awali, Mratibu wa Tapanet, Tolbert Mmasy alisema mradi huo wa miaka minne utagharimu sh milioni 400 na unalenga kusaidia kutoa taarifa sahihi kwa shughuli za wasaidizi wa kisheria na kuhakikisha jamii inapata haki sawa pale inapotokea tatizo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: