BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Edward Lowassa atii sheria bila shuruti, awasili makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania

Dar es Salaam. Msafara wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ukiwa na magari manne ukisindikizwa na magari mawili ya polisi umewasili makao makuu ya polisi.

Jana Lowassa alipewa taarifa ya kwenda kuhojiwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Mapema leo, Jumanne asubuhi polisi wameimarisha ulinzi katika barabara zote zinazoingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Mtaa wa Ohio.

Polisi wakiwa na silaha wameegesha magari yao kwenye kila barabara inayoingia makao makuu ya jeshi hilo, huku wengine wakizunguka zunguka maeneo ya jirani. 


Wananchi wanaruhusiwa kupita lakini walio kwenye vikundi wanasimamishwa na kuhojiwa, huku wengine wakizuiwa kabisa kukatiza eneo hilo.Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment