BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HONG KONG SI LOLOTE SI CHOCHOTE BAADA YA KUANGUKIA PUA MBELE YA ANGOLA KWA MIJI GHALI ZAIDI DUNIANI


Mji mkuu wa Angola, Luanda umechukua nafasi ya kwanza kama mji ghali zaidi duniani kwa wataalamu na kuusukuma mji wa Hong Kong hadi nafasi ya pili.

Hii imetokana na takwimu za gharama ya kuishi kutoka na utafiti ulifanywa na shirika la Mercer

Miji ya Tokyo, Zurich na Singapore pia nayo inachukua nafasi tano za kwanza.

Mji wa London ulishuka hadi nafasi ya 30 hasa kutokana na kushuka kwa thamani ya pauni.

Utafiti huo wa kila mwaka huangazia masuala kadha kando na gharama ya kukodi nyumba.

Utafiti huo huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji, ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi, chakula na burudani.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment