BannerFans.com

WANAFUNZI 60 WA SEKONDARI CHITA WAGEUZA MAGOTI MEZA, NI BAADA YA KUKOSA MADAWATI KILOMBERO

Millionaire  Ads

MWANAUME ALAZIMISHWA KULIPA MAHALI BAADA YA MCHUMBA WAKE KUFARIKI DUNIA DOLA 800

 
Mtu mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikendi iliopita kulingana na chombo cha habari cha taifa.

Baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua ,nduguze walimlazimisha mpenziwe kulipa ''Lobolo'', wakionya kwamba la sivyo hatozikwa.

Ndugeze walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafikia majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya janga hilo kutokea.

Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 na kufanya haruasi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.

Nduguye kijana huyo Irmao do Jovem alielezea matatizo yao.

''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha dola 178 pekee.Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi''.

Huku ikiwa familia ya kijana huyo imekubali kulipa,walishutumu tabia ya familia ya mwanamke huyo.

Hatahivyo, ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Mozambique hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads