BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAUAJI YANAENDELEA ?, WATATU WAUAWAWA KWA KUPIGWA RISASI WILAYA YA KIBITI


Pwani. Habari zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa watu watatu wakazi wa kijiji cha Nyamisati, wilayani Kibiti wanadaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Mkazi mmoja wa Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamza amesema miongoni mwa watu waliopigwa yumo mwanamke mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji kimojawapo kijijini hapo.

Wanaosadikiwa kupoteza maisha ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela.

Mkuu wa wilaya ya Kibiti Gullamuhusein Kifu amesema ameliagiza jeshi la Polisi wilayani hapa kwenda eneo hilo kwa ajili ya uthibitisho/Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: