BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BUNGE LASHAMBULIWA KWA RISASI ZA MOTO


Askari wa Jeshi la Iran wakijihami wakati wa shambulio katika Bunge la Iran katikati ya Tehran juzi.


KUNDI la watu wenye silaha limelishambulia Bunge la Iran na jengo lenye kaburi la mwasisi wa mapinduzi ya Kiislamu ya taifa hilo na kuua watu 12 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Kwa mujibu ya mashirika ya habari ya ISNA na Fars, washambuliaji kadhaa waliingia bungeni kupitia lango la Kaskazini na mmoja wa waliojeruhiwa ni mlinzi wa Bunge.

Mbunge mmoja ameliambia Shirika la Habari la IRIB kuwa jumla ya washambuliaji wanne waliingia bungeni wakiwa wamebeba bunduki na bastola.

Aidha katika shambulio jingine, mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliingia katika jengo lenye kaburi la mwanzilishi wa mapinduzi ya Iran, Ruhollah Khomeini, akafyatua risasi kadhaa kabla ya kujilipua mwenyewe.

ISNA limesema walioshambulia Bunge wamezingirwa, lakini bado hawajakamatwa.

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) limedai kuhusika na mashambulizi hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: