BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS DK MAGUFULI AOMBEWA DUA UWANJA WA JAMHURI YA KUMKINGA NA MAADUI MOROGORO

Sheikhe mkuu wa mkoa wa Morogoro, Abdallah Mkangambe akiomba dua ya kumuombea rais Dk John Magufuli aepukane na maadui iliyofanyika kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro, wa kwanza kushoto ni Kamanada wa polisi Morogoro, Ulrich Matei, Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood na Mchungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Emmanuel Tengeneza.

Juma Mtanda, Morogoro.
Wakazi wa Morogoro wameungana na viongozi mbalimbali kumuombea dua Rais, Dk John Magufuli ili aendelee kuwa na afya njema na nguvu katika juhudi za kupambana na watu wachache wanaodhohofisha uchumi wa nchi.

Dua hiyo ilikuwatanisha viongozi wa dini, wazee wa mila, vyama vya siasa na serikali na kufanyika uwanja wa jamhuri kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana.

Akizungumza wakati wa dua hiyo, Sheikhe wa mkoa wa Morogoro, Abdallah Mkangambe aliomba kwa kusema kuwa wanamuomba mwenyezi mungu kumjalia Rais Magufuli kumpa nguvu na ujasili ili amani inayoambatana na uchumi.

Mkangambe alisema kumkinga rais na watu wabaya, wenye nia mbaya na Tanzania ili aweze kushinda ndani na nchi.

“Tunamuomba mwenyezi mungu aendelee kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha amani lakini awajalie viongozi wengine kuwa na nguvu, ujali, hekima na busara ili watu wenye tabia za kiufisadi wapate hofu na kuacha matendo hayo.”alisema Sheikhe Mkangambe.

Mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT), Emmanuel Tengeneza alisema kuwa rais amekuwa akifanya kazi njema na wanategemea mwenyezi mungu atamlinda dhidi ya maadui wa Tanzania.

Mchungaji Tengeneza alisema kuwa amemchagua rais na kumlinda na wanamuomba mwenyezi mungu na amuwekee roho mtakatifu ili aweze kuvunja nguvu zote za maadui zake na viongozi wa vyama vya siasa na serikali.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Morogoro (CCM), Innocent Kalogeris alisema kuwa rais Magufuli amepigana vita nyingi lakini amewaomba watanzania wamuombee kwa mwenyezi mungu ili aendelee kupambana na maadui wa Tanzania ili isonge mbele.

Kalogeris alisema kuwa rais amekuwa akipigana vita lakini Tanzania inahitaji inapanda kiuchumi, mshikamano, umoja na inahitaji maombezi ya mungu na ni wajibu wao kumuombea dua njema.

“Tunadhamira ya dhati ya kumuombea rais Magufuli dua njema kwa mwenyezi mungu lakini na viongozi wengine wa chama na serikali awape afya njema, busara, hekima na maarifa katika kazi zao za kila siku katika ngazi zote…amina.”alisema Kalogeris.

Viongozi waliohudhuria hafla hiyo ya dua ni pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Morogoro, mkuu wa wilaya ya Morogoro, viongozi wa dini mbalimbali na wananchi wa kawaida.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: