BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC YATOLEWA NISHAI NA TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA KENYA MASHINDANO YA SPORTPESA CUP 2017

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imeaga mashindano ya SportPesa Cup baada ya kukubali kipigo cha bao 5-4 kutoka kwa Nakuru Stars ya Kenya kwa changamoto ya mikwaju ya penalti katika mchezo mkali uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Hatua hito ya penalti ilichukuliwa baada ya kumalizika dakika 90 za mchezo kwa sare ya 0-0 ambapo katika mikwaju hiyo ya penalti Simba SC ilifanikiwa kupata minne huku Nakuru Star iliyopo ligi daraja la kwanza nchini Kenya ikipata mikwaju mitano na kuiondosha Simba SC katika michuano hiyo.
PENALTI 5
Klabu ya Simba SC ya Tanzania.
Bukungu 1.
Daniel Agray X.
Mwinyi Kazimoto 3.
Hafidhi Mussa 4.
Festoni Munesro 5

PENALTI 5.
Nakuru Star ya Kenya.
Ntorokundo Baraka 1. Tz
Amani Kiata 2.Tz
Maina Kagete 3.
Amakanji Ekuba 4.
Ng'ang'a Kamaru 5.

Katika mchezo ulionza mapema majira ya saa 8 mchana, Gol Mahia ya Kenya na yenyewe imeisambaratisha klabu ya Jang'ombe Boys ya Zanzibar kwa kuitandika bao 2-0 na kuindosha kwenye kinyang'anyiro hicho.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment